Video: Majonzi yamfanya mke wa Papa Wemba ashindwe kuzungumza kwenye tuzo za Afrima
Kwenye tuzo za Afrima 2016 zilizotolewa Jumapili, jijini Lagos, Nigeria,
marehemu Papa Wemba ni miongoni mwa wasanii nguli wa Afrika waliopewa
tuzo ya heshima. Kupokea tuzo hiyo, alikuwepo mke wake pamoja na mwanae
wa kike. Hata hivyo mjane huyo alishindwa kabisa kuongea chochote kutokana na
kuwa na huzuni kubwa. Bintiye alimwakilisha na kushukuru kwa upendo
mkubwa kutoka kwa Waafrika tangu kifo chake. Alidai kuwa wamejiwekea
nadhiri kumuenzi Papa Wemba kila siku katika maisha yao. Mwanae huyo pia
alitumia fursa hiyo kuimba wimbo wa baba yake.
Post a Comment