FC ROSTOV YAIPATIA KIPIGO CHA KUSHTUKIZA BAYERN MUNICH

Timu ya Bayern Munich itamaliza katika nafasi ya pili katika Ligi ya Mabingwa Ulaya kundi D baada ya kupata kipigo cha kushtukiza cha magoli 3-2 kutoka kwa FC Rostov ya Urusi.

Timu hiyo ya Ligi Kuu ya Urusi ilipata ushindi wake huo wa kwanza kati Ligi ya Mabingwa Ulaya katika mchezo huo uliochezwa kwenye hali ya hewa ya nyuzi joto -4.

Kwa matokeo hayo FC Rostov inakuwa timu ya kwanza ya Urusi kuwahi kuifunga timu kubwa ya ligi ya Bundesliga katika Ligi ya Mabingwa Ulaya.
 Cristian Noboa akishangilia goli lake la mpira wa adhabu lililofanya matokeo kuwa 3-2
Katika mchezo mwingine Atletico Madrid imeibuka na ushindi wa magoli mawili kwa bila dhidi ya PSV Eindhoven, magoli yaliyofungwa na Gameiro na Griezmann.

No comments

Powered by Blogger.