Vigogo wa Jeshi la Polisi Wakamatwa na Magari Matatu ya Wizi
Wakazi wa Mji mdogo wa Himo
wilayani Moshi wameshangazwa na kitendo cha Jeshi la Polisi mkoani humo
kutowachukulia hatua maofisa wake wawili wanaohusishwa na mtandao wa
wizi wa magari.
Maofisa hao wawili wanaotuhumiwa, mmoja
anacheo cha Mrakibu wa Polisi (ASP) na mwingine Koplo walikamatwa na
magari matatu ambayo waliyasafirisha hadi jijini Dar es Salaam.
Taarifa kutoka ndani ya Polisi zinaeleza
kuwa maofisa hao walikamatwa na kikosi kazi maalum kutoka Dar es Salaam
tangu mwezi uliopita lakini hadi leo hakuna hatua yoyote
iliyochukuliwa.
Katika operesheni hiyo, mtuhumiwa
mwingine ambaye ni raia alikamatwa nyumbani kwa Koplo huyo akiwa na gari
moja la wizi na vibao vya namba za magari 70.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro,
Wilbroad Mtafungwa alipoulizwa na gazeti la Mwananchi alikiri maofisa
hao kukamatwa na magari hayo akasema lakini mtu hawezi kupewa adhabu
kabla ya kuthibitika kuwa kafanya uhalifu.
Post a Comment