Ombi la Meya wa Jiji la Dar Kuhusu Mgogoro wa UDA na Jiji
MWANDISHI WETU, Dodoma
MEYA
wa jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita ameiomba Kamati ya Bunge ya kudumu
ya Hesabu za Serikali LAAC kuona namna ambavyo wanaweza kuisaidia ili
mgogoro uliopo baina ya Jiji la Dar es Salaam na Kampuni ya Usafirishaji
ya Dar es Salaam UDA unamalizika.
Hatua
hiyo imekuja baada ya majadiliano ya muda mrefu baina ya wajumbe wa
kamati na watendaji wa jiji kushindwa kufikia muafaka juu nani hasa
Mmiliki wa kampuni hiyo, sambamba na uwepo wa mwanahisa Saimoni group
ambaye ndiye Mwenye hisa nyingi ndani ya Kampuni hiyo.
Meya
Isaya alieleza kwamba iwapo kamati hiyo itaingilia Kati Jambo hilo
itawezesha pesa ambazo zipo Benki kuu ambazo zilitokana na hisa za
shirika hilo kiasi cha billion 5.9 zielekezwe kwenye matumizi mengine
kwa ajili ya maendeleo ya jiji la Dar es Salaam.
Alifafanua
kwamba pesa hizo hadi sasa bado zipo Benki kuuu na kwamba katika kikao
cha baraza la madiwani la Jiji Iililo kaa Aprili 22 mwaka huu lilishauri
kwamba pesa hizo zisitumike hadi pale jiji litakapo pata ushauri kutoka
kwa mwanasheria Mkuu wa serikali George Masaju.
"
Ndugu Mwenyekiti wa kamati , na wajumbe wa kamati hii, jambo hili
linatupa wakati mgumu sana, mana pesa ambazo zipo zingefaa kufanya mambo
mengine ya Maendeleo, lakini unashindwa, sasa niwaombe tu jambo hili
mlichukue tunataka liishe .
Kama
baraza liliuliza kuhusu pesa hizo, nakuona kwamba tuombe ushauri kutoka
kwa mwanasheria Mkuu wa serikali ,na sisi tulikuwa tunasubiri ushauri
kutoka kwake, sasa kwakuwa tayari limeshafika kwenu, tunaomba
muliangalie kwa nafasi yenu "aliongeza.
Awali
taarifa ya mkaguzo mkuu na mthibiti wa Hesabu za Serikali CAG ilieleza
kwamba haitambu mchakato mzima wauuzaji wa shirika hilo la UDA kutokana
na kwamba mchakato huo haukuwa wa kihalali na badala yake uliendeshwa
kinyemela.
Kwa
upande wake wajumbe wa kamati hiyo waliuliza uwepo wa mwanahisa Simon
Group ndani shirika hilo, ambapo Mkurugenzi wa Jiji alosema kwamba
hafahamu na kwamba hata yeye anashangaa jambo hilo hadi kesho.
"Ndugu
Mwenyekiti wa kamati na wajumbe wa kamati hii , nikiulizwa kwanini
Simon Group yupo hapa, sina majibu na kwamba mwenyewe naendelea
kushangaa hadi kesho kuwepo kwake, sasa sijui
Kwa
upande wake Mwenyekiti wa kamati hiyo Abdala Chikota alisema kwamba
kutokana na majibu ambayo yametolewa , Meya wa Jiji, Katibu Tawala wa
mkoa , Mkurugenzi wa Jiji na timu nyingine wafike tena kwenye kamati
hiyo Oktoba 28 ambapo waziri wa nchi Ofisi ya Raisi Tawala za mikoa na
Serikali za mitaa kufika kwa ajili ya kuangalia namna ambayo wanamaliza
jambo hilo.
Chikota
alisema anafahamu mlolongo mzima wa jambo hilo na kwamba wanasubiri
maelezo ya waziri George Simbachawene ili kuona namna gani ambavyo jambo
hilo litamalizika.
Post a Comment