Akizungumza na Mhe. Makonda.
Mapema leo Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ametoa majibu
kuhusu na hatma ya kijana Said Ally aliyetobolewa macho na Scorpion
maeneo ya Buguruni Sheli na kusema hatoweza kuona tena.
Akizungumza na waandishi wa habari mkuu huyo wa mkoa amesema:
“Majibu yametoka na Said ameturuhusu tuyaweke wazi majibu ni mabaya
ila tumeyapokea itabidi tukubaliane na matokeo kwamba ndugu yetu
hataweza kuona tena kwa maisha yake yote.
“Serikali ya mkoa imejitolea kumpatia matibabu ya macho ya bandia kwa
ajili ya kutengeneza shape ya uso wake tena, kumpatia elimu ya kusoma
tena kujifunza kwa alama ili aweze kuendana na mazingira. Serikali ya
mkoa imetoa gari kwa ajili ya kumsaidia kipindi chote atakachokuwa
kwenye matibabu yake.
“Kabla ya kupatwa na ulemavu huo, Said alikuwa kinyozi hivyo kuna
mdogo wake yupo atamsaidia kwakuwa mwanzoni walikuwa wakifanya kazi
pamoja.”
Na Hilaly Daud/ GPL
| | | | | | |
Post a Comment