SERIKALI IMESITISHA SUALA LA MABADILIKO YA UKODISHWAJI NA UWEKEZAJI NDANI YA YANGA, SIMBA
Serikali imetangaza kuzuia mchakato wa ukodishwaji na uwekezaji ndani ya klabu za Yanga na Simba.
Yanga
tayari ilikuwa imemkodisha Yusuf Manji kwa miaka 10 na Simba ilikuwa
katika harakati za kumuuzia hisa 51 Mohammed Dewji, sasa yote
hayatafanyika,
Taarifa
iliyotolewa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) kupitia katibu mkuu wake,
Mohamed Kiganja imesitisha zoezi hilo hadi hapo klabu hizo zitakapofanya
mabadiliko katika katiba zao.
Katika
taarifa ya Kiganja, imesema zoezi hilo limesitishwa hadi matekebisho ya
klabu zote mbili kupitia sheria ya msajili wa michezo namba 442, kanuni
ya 11 kifungu kidogo cha (1-9).
Pamoja
na kueleza hilo, mwishoni taarifa hiyo inaonyesha wazi kwamba serikali
haitaki mchakato huo baada ya kusema mjadala umefungwa lakini
inasisitiza wanaotaka kumiliki timu zao, basi wafanye juu chini kumiliki
klabu zao kama alivyoamua kufanya Said Salim Bakhresa.
Post a Comment