PICHA: Tunda Man Afunga Ndoa
…Dogo Janja akiwa na shemeji yake.
Madee akipiga picha ya kumbukumbu na shemeji yake.
…Picha ya pamoja na baadhi ya marafiki.
…Akimpatia pesa mkewe.
MWANAMUZIKI wa kizazi kipya nchini kutoka
kundi la TipTop Connection, Tunda Man amefunga ndoa na mchumba wake wa
muda mrefu Bi Sabra, ndoa ya wawili hao imefungwa kwenye Msikiti Mkuu wa
barabara ya Boma, mjini Morogoro.
Mkali huyo wa wimbo uitwao ‘Mama Kijacho’
amefunga ndoa hiyo siku ya jana Ijumaa na kuhudhuriwa na baadhi ya
marafiki zake wa karibu akiwemo Madee, Dogo Janja na Kassim Mganga.
Kabla ya ndoa hiyo kufungwa ilitanguliwa na sherehe ya kuagwa binti
‘Send-off’ iliyofanyika juzi alhamisi.
Kwa mujibu wa shuhuda wetu aliye mjini
Morogoro, sherehe hiyo ya harusi inaendelea kwa siku ya tatu leo
nyumbani kwa bibi harusi.
Post a Comment