LIONEL MESSI AREJEA DIMBANI KWA KUFUNGA GOLI WAKATI BARCELONA IKIUWA 4-0

 Lionel Messi amerejea dimbani baada ya kupona kwa kufunga goli katika mchezo wa La Liga wakati Barcelona ikipata ushindi kirahisi wa magoli 4-0 dhidi ya Deportivo La Coruna katika dimba la Nou Camp.

Mshambuliaji huyo wa Argentina amerejea dimbani baada ya kuwa nje kwa wiki tatu, akikabiliwa na maumivu ya nyonga, aliifungia Barcelona goli la nne sekunde kadhaa baada ya kutokea benchi.

Alikuwa Rafinha aliyeanza kuwafungia wenyeji goli la kwanza na kisha baadaye akaongeza la pili katika kipindi cha kwanza, kabla ya Luis Suarez kufunga kwa ufundi goli la tatu la Barcelona.
Kwa ushindi huo timu ya Barcelona imepanda hadi katika nafasi ya pili ya msimamo wa ligi hiyo ambayo kwa sasa inaongozwa na Sevilla, huku Real Madrid ikiwa katika nafasi ya tatu.
                            Rafinha akifunga goli lake la pili katika mchezo huo
                                       Lionel Messi akifunga goli la nne la Barcelona

No comments

Powered by Blogger.