Baada ya kushindwa kufanya vyema na
timu ya taifa ya Uingereza, Theo Walcott ameendeleza makali yake
akiwa na Arsenal na kuisaidia kuibuka na ushindi wa magoli 3-2 dhidi
ya Swansea katika mchezo wa Ligi Kuu ya Uingereza.
Mshambuliaji huyo wa Arsenal na
Uingereza sasa ana magoli matano katika michezo minane, alifunga goli
la kwanza kufuatia makosa ya Jordi Amat na kisha kuongeza la pili
kupitia mpira wa kichwa uliopigwa vibaya na Jack Cork.
Swansea wakiwa na kocha wao mpya Bob
Brandley walionekana kupoteza matumaini baada ya magoli hayo, hadi
pale Gylfi Sigurdsson alipofunga goli kufuatia makosa yaliyofanywa na
Granit Xhaka na kuwapa matumaini.
Mesut Ozil aliifungia Arsenal goli
la tatu kufuatia krosi iliyopigwa na Alexis Sanchez, hata hivyo
mchezaji aliyetokea benchi Borja Baston aliiunganisha wavuni krosi
iliyopigwa kiufundi na Modou Barrow na kufunga goli la pili.
Theo Walcott akishangilia goli lake la kwanza alilolifunga katika mchezo huo
Borja Baston akifunga goli la pili la Swansea na kuipa presha Arsenal
Post a Comment