Mahakama Yamfutia Shtaka la Unyang’anyi wa Kutumia Silaha Scorpion
Salum Njwete maarufu kwa jina la Scorpion akiwa chini ya ulinzi (Picha na Maktaba).
Mahakama ya Wilaya Ilala jijini Dar es Salaam leo imemfutia shtaka la
unyang’anyi wa kutumia silaha, Salum Njwete maarufu kwa jina la
Scorpion baada ya upande wa mashtaka kuomba shtaka hilo
liondolewe mahakamani hapo kwa sababu hawana nia ya kuendelea na kesi
hiyo.Mtuhumiwa huyo ambaye ni mkazi wa Buguruni kwa Mnyamani anatuhumiwa kumchoma visu na kisha kumtoboa macho, Said Ally mkazi wa Mabibo Hostel hivi karibuni.
Post a Comment