Bodi ya Wadhamini CUF yafungua kesi dhidi ya Jaji Mutungi na Mwanasheria Mkuu wa Serikali
BODI
ya Baraza la Wadhamini la Chama cha Wananchi (CUF), imefungua kesi
dhidi ya Jaji Francis Mutungi, George Masaju, Profesa Ibrahimu Lipumba
na wafuasi 12 waliotimuliwa na chama hicho katika Mahakama Kuu ya
Tanzania.
Jaji
Mutungi ni Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Masaju ni Mwanasheria
Mkuu wa Serikali (AG) na Prof. Lipumba ni Mwenyekiti wa CUF
anayetambuliwa na Msajili wa Vyama vya Siasa.
Bodi hiyo imefungua kesi hiyo ikiwa ni wiki chache baada ya mahakama hiyo kutoa kibali cha kufungua kesi dhidi yao.
Kibali
hicho kilitolewa mbele ya Jaji Ama Isario Munisi ambapo alisema,
mahakama ilijiridhisha kwamba, maombi ya bodi hiyo yaliyokuwa na hati ya
kiapo cha Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad zipo sahihi,
hivyo wanapaswa kufungua kesi hiyo ndani ya siku 14.
Hatua
ya bodi kukimbilia mahakamani inatokana na kuibuka kwa mgogoro ndani ya
chama hicho baada ya Prof. Lipumba kutangaza kujiuzulu nafasi ya
Uenyekiti Agosti 6, mwaka jana na Juni mwaka huu, kutangaza kutengua
barua yake na kisha kurejea kwenye wadhifa wake.
Bodi
hiyo inayowakilishwa na mawakili zaidi ya 10 akiwemo Juma Nassoro,
Hashimu Mziray na Twaha Taslima leo wamefanikiwa kufungua kesi
iliyopokelewa na kupatiwa namba 23 ya mwaka 2016 chini ya hati ya
dharura.
Akizungumza
na waandishi wa habari baada ya kufungua kesi hiyo, Wakili Mziray
amesema msingi wa kesi yao umejengwa katika hoja kubwa tatu ambazo;
Bodi
imeiomba Mahakama Kuu kutengua barua ya Jaji Mutungi ya Septemba 23,
mwaka huu iliyotengua uamuzi halali wa CUF, kumfuta uanachama Prof.
Lipumba.
Pia
bodi inaiomba mahakama hiyo kumzuia Jaji Mutungi kuendelea kufuatilia
suala la CUF baada ya kupitishwa kwa uamuzi wa kumfuta uanachama Prof.
Lipumba kwa kuwa, suala lake limefanyika kihalali.
Aidha
katika hoja ya tatu, wanaiomba mahakama kumzuia rasmi Jaji Mutungi
kutoingilia masuala yanayoihusu CUF, badala yake afanye kazi
zinazomuhusu kisheria.
Badaa
ya kueleza hayo, Wakili Mziray amesema sababu ya kufungua kesi hiyo
chini ya hati ya dharura inatokana na hatari iliyopo ndani ya chama
hicho.
“Licha
ya kuwa kuna mambo yaliyotokea ndani ya chama, lakini kuna sababu ya
kufungua kesi chini ya hati ya dharura kutokana na Ofisi Kuu ya chama
pale Buguruni imekaliwa na watu ambao sio wanachama,”anasema na
kuongeza;
“Lengo
la chama ni kudhibiti ofisi zake zote katika hali ya usalama ikiwemo
Makao Makuu, kwani Kaimu Katibu Mkuu anahitaji kusimamia kazi na
shughuli za chama akiwa huru.”
Mbarara
Maharagande, aliyeteuliwa kushika nafasi ya Unaibu Mkurugenzi wa
Habari, Uenezi na Mahusiano wa CUF amesema kuwa, chama hicho
kinasikitishwa na utendaji kazi wa Jeshi la Polisi kwa kuwalinda na
kuwaachia wahalifu wanaoivuruga CUF, badala yake inawakamata
wasiohusika.
“Tunashangaa
kuona polisi wanaharakisha kuwafikisha mahakamani wafuasi 23 waliokuja
kuongeza nguvu ya kukilinda chama wakitokea Zanzibar, huku wakishindwa
kuwachukuliwa hatua waliofanya tukio la utekaji ambalo ndio la kwanza
kutokea,” anasema.
Maharagande
anasema kutokana na hatua hiyo, asubuhi ya leo viongozi wa chama hicho
wamekwenda Ofisi za Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP), Biswaro Mganga
kuulizia hatma ya wafuasi waliohusika na tukio la utekaji iwapo
wamechukuliwa hatua.
“Licha
ya kufika ofisi hapo tumeshangazwa kuona hata kwenye orodha ya jalada
la kesi za leo hakuna majina ya washtakiwa hao, licha ya kuwa
wamekamatwa muda mrefu lakini wameshindwa kuchukuliwa hatua,” amesema
Post a Comment