Hatimaye Kocha Mkuu wa Yanga Awaaga Wachezaji na Benchi la Ufundi
HATIMAYE ikiwa ni siku moja baada ya
aliyekuwa Kocha Mkuu wa klabu ya Dar es Salaam Young Africans, Hans van
Pluijm aandike barua ya kujiuzulu nafasi yake hiyo, baada ya kusikia
kuwa kuna kocha kutoka Zesco United ya Zambia, George Lwandamina amekuja
tayari Tanzania kuchukua nafasi yake, leo Oktoba 25 amewaaga rasmi
wachezaji wake na benchi la ufundi.
Hans amewaaga wachezaji wake pamoja na
benchi la ufundi katika mazoezi ya leo asubuhi yaliofanyika katika
uwanja wa Polisi Kilwa Road, kocha Hans anaondoka Yanga akiwa kaipa
mafanikio makubwa ikiwemo kukushiriki hatua ya Makundi ya Kombe la
shirikisho barani Afrika CAF, hatua ambayo Yanga wana miaka mingi toka
waifikie.
Post a Comment