Waziri
wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Dkt. Charles Mwijage akizungumza na
wadau mbalimbali wa maendeleo na Viongozi waandamizi wa Serikali wakati
wa uzinduzi wa matokeo ya sensa ya uzalishaji viwandani ya mwaka 2013
leo Oktoba 17, 2016 Jijjini Dar es Salaam.
Baadhi
ya Maafisa Wandamizi wa Serikali kutoka Wizara ya Viwanda, Biashara na
Uwekezaji, na Ofisi ya Taifa ya Takwimu wakifuatilia mada mbalimbali
zilizokuwa zikiwakilishwa wakati wa uzinduzi matokeo ya sensa ya
uzalishaji viwandani ya mwaka 2013 leo Oktoba 17, 2016 Jijjini Dar es
Salaam.
Baadhi
ya wawakilishi kutoka taasisi mbalimbali nchini wakifuatilia mada
mbalimbali zilizokuwa zikiwakilishwa wakati wa uzinduzi matokeo ya sensa
ya uzalishaji viwandani ya mwaka 2013 leo Oktoba 17, 2016 Jijjini Dar
es Salaam.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Dkt. Adelhelm Meru
akizungumza wakati wa uzinduzi wa matokeo ya sensa ya uzalishaji
viwandani ya mwaka 2013 leo Oktoba 17, 2016 Jijjini Dar es Salaam.
Waziri
wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Dkt. Charles Mwijage (katikati)
akifuatilia mada mbalimbali zilizowasilishwa na wadau mbalimbali wakati
uzinduzi wa matokeo ya sensa ya uzalishaji viwandani ya mwaka 2013 leo
Oktoba 17, 2016 Jijjini Dar es Salaam. Wengine katika picha kutoka kulia
ni Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Dkt. Albina Chuwa
|
Waziri
wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Dkt. Charles Mwijage (kulia) akiteta
jambo na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Adelhelm Meru wakati wa
uzinduzi wa matokeo ya sensa ya uzalishaji viwandani ya mwaka 2013 leo
Oktoba 17, 2016 Jijjini Dar es Salaam. |
|
Baadhi
ya Maafisa Wandamizi wa Serikali kutoka Wizara ya Viwanda, Biashara na
Uwekezaji, na Ofisi ya Taifa ya Takwimu wakifuatilia mada mbalimbali
zilizokuwa zikiwakilishwa wakati wa uzinduzi matokeo ya sensa ya
uzalishaji viwandani ya mwaka 2013 leo Oktoba 17, 2016 Jijjini Dar es
Salaam.
Waziri
wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Dkt. Charles Mwijage akiwa ameshika
vitabu mbalimbali vya taarifa ya utafiti kuhusu matokeo ya sensa ya
uzalishaji viwandani ya mwaka 2013 leo Oktoba 17, 2016 Jijjini Dar es
Salaam.
Waziri
wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Dkt. Charles Mwijage (kushoto)
akimkabidhi taarifa ya kitabu cha utafiti kuhusu matokeo ya sensa ya
uzalishaji viwandani ya mwaka 2013 kwa Mwakilishi Mkazi wa Shirika la
Umoja wa Mataifa linaloshughulikia viwanda (UNIDO), Gerald Runyoro leo
Oktoba 17, 2016 Jijjini Dar es Salaam (PICHA NA ISMAIL NGAYONGA-
MAELEZO)
Na Beatrice Lyimo, MAELEZO-Dar es Salaam
SERIKALI
imeitaka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) kwa kushrikiana na wadau wa
maendeleo nchini ikiwemo Shirika la Maendeleo ya Viwanda Duniani (UNIDO)
na Shirikisho la Viwanda Nchini (CTI) kuendelea kufanya utafiti ili
kubaini idadi na maendeleo ya viwanda vidogo vilivyopo nchini.
Hayo
yamesemwa leo Jijini NA Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Dkt
Charles Mwijage wakati wa uzinduzi wa matokeo ya Sensa ya Uzalishaji
bidhaa Viwandani mwaka 2013.
Dkt Mwijage alisema kuwa katika
mataifa yanayoendelea duniani ikiwemo Korea Kusini, Malaysia na
Singapore uchumi wa nchi hizo umeweza kukua kwa kiwango kwa juu zaidi
kutokana na kuweka mkazo katika kuendeleza viwanda vidogo na vya kati.
Alisema
katika kuharakisha kasi ya maendeleo ya vidogo yanapatikana nchini,
Wizara yake imekusudia kuwajengea hamasa Watanzania kupendelea kujenga
viwanda vidogo vidogo na vya kati, kwani kukua kwa sekta ya viwanda
nchini kutaisaidia kuinua uchumi wan chi.
“Asilimia 25- 40 ya
mazao ya kilimo yanayovunwa huharibika kabla ya kufikishwa kiwandani,
katika kukabiliana na hali hiyo Serikali imekusudia kujenga viwanda
vidogo vidogo ili kuwawezesha wakulima wapate sehemu nzuri zaidi za
kuhifadhi mazao yao” alisema Mwijage.
Aidha, Dkt Mwijage
alisema, sekta ya viwanda vidogo vidogo nchini imeendelea kukua kwa kasi
nchini ambapo hadi sasa kuna jumla ya viwanda 3800 vilivyoanzishwa
nchini kuanzia Novemba 2015 hadi octoba, 2016.
Katika hatua hiyo
Dkt Mwijage alisema kuwa Wizara yake inaendelea kuhamasisha Sekta
binafsi kuwekeza katika Sekta ya viwanda vidogo, vya kati na vikubwa
ikiwa jukumu kuu la Serikali ni kuhakikisha nchi inakuwa salama na
inajenga mazingira wezeshi kwenye sekta binafsi kuzalisha na kufanya
biashara.
Naye Mkurugenzi Mkuu Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS)
Dkt Albina Chuwa alisema kuwa matokeo hayo yanaonyesha mafanikio katika
sekta ya viwanda ikiwemo kuongezeka kwa ajira zipatazo 264,223 nchini na
kuchangia uchumi kwa takribani Shilingi bilioni 8.0 kwa mwaka 2013.
Alisema
kuwa Takwimu za matokeo ya sense ya uzalishaji viwandani ni rasmi na
kuwataka watunga sera, wanasiasa, viongozi, sekta binafsi na watu
binafsi kutumia matokeo hayo kwa lengo la kuboresha Sekta ya viwanda
nchini.
|
Post a Comment