SERENA WILLIAMS AJITOA KUSHIRIKI FAINALI ZA MCHUNANO YA TENESI YA WTA

Serena Williams amejitoa kushiriki fainali za mchunano ya tenesi ya WTA wiki ijayo nchini Singapore kutokana na kuwa na jeraha la kwenye bega.

Mmarekani huyo namba mbili duniani katika mchezo huo, hakucheza tangu atinge nusu fainali za michuano ya wazi ya Marekani mwezi Septemba.

Nafasi ya Williams sasa itaenda kwa Muingereza, Johanna Konta, ambaye anashika nafasi ya tisa katika mchezo huo, ingawa naye alikuwa na maumivu ya tumbo.

No comments

Powered by Blogger.