Arturo Vidal na Douglas Costa
wamecheka na nyavu wakati Bayern Munich ikiibuka na ushindi wa
magoli 2-0 dhidi ya Borussia Moenchengladbach 2-0.
Matokeo hayo yameifanya Bayern
kupata ushindi wao wa kwanza katika mechi tatu za Bundesliga
walizocheza na kuisaidia kuongoza ligi hiyo kwa tofauti ya pointi
tatu.
Wageni Borussia Moenchengladbach
walitarajiwa kutoa upinzani mkali baada ya kupata ushindi katika Ligi
ya Mabingwa Ulaya dhidi Celtic, lakini wakajikuta wanageuziwa kibao.
Arturo Vidal akiwa amepiga mpira ulioazaa goli la kwanza la Bayern Munich
Douglas Costa akishangilia kwa kujipiga selfie na mashabiki baada ya kufunga goli la pili kwa Bayern Munich
Post a Comment