YANGA wanaendeleza ule msemo wa kuwa wao ni wa kimataifa kwa kupiga masafa anga kwa anga, hiyo ni baada ya kuamua kukodisha ndege maalum kutoka Pemba kuelekea Dar es Salaam kuwavaa watani wao wa jadi, Simba, kesho Jumamosi. Ishu ipo hivi, Yanga walitoka Shinyanga, Jumatatu ya wiki hii wakitoka kuvaana na Stand United, wakapanda ndege kurejea Dar es Salaam, kisha wakaunganisha kwenda Pemba kwa ndege kuweka kambi kwa ajili ya mechi hiyo ya Ligi Kuu Bara. Taarifa ambazo imezipata Championi Ijumaa ni kuwa Yanga imepanga kurejea Dar, leo Ijumaa jioni mara baada ya mazoezi ya asubuhi watakayofanya kwenye Uwanja wa Gombani na kurejea hotelini kupumzika kisha jioni kupanda ndege hiyo. Hatutaki kuona wachezaji wetu wakipata uchovu wa safari na ndiyo sababu ya sisi kutumia ndege katika safari zetu, kama unakumbuka tulienda Shinyanga na ndege, tukarudi Dar na ndege kabla ya kubadilisha nyingine kuelekea Pemba. Timu yetu ipo vizuri, tunashukuru kikosi chetu kipo fiti kwa maana ya kutokuwa na majeruhi kwa wale waliokuwepo, alisema mtoa taarifa huyo
Post a Comment