Waziri Mkuu Kuongoza Kuagwa Waliokufa kwa Tetemeko Bukoba
Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa leo
anatarajiwa kuongoza waombolezaji kuaga miili ya watu 16 waliopoteza
maisha kwenye tetemeko la ardhi lililotokea jana mkoani Kagera.
Zoezi hilo la kuaga miili linafanyika katika Uwanja wa Kaitaba uliopo Bukoba Mjini mkoani Kagera.
Jumla ya watu 16 wamefariki dunia huku zaidi ya 200 wakijeruhiwa.
Zifuatazo ni picha za waombolezaji pamoja na miili ya waliopoteza maisha ikiwasili Uwanja wa Kaitaba;

Picha kwa hisani ya Bukoba Wadau
Post a Comment