Video: Wema Awatimua Team Wema
Muigizaji nyota wa filamu nchini, Wema Sepetu.
Muigizaji nyota wa filamu nchini, Wema Sepetu amewatimua watu wanaojiita Team Wema waliotapakaa katika mitandao mbalimbali ya kijamii, akisema hawataki kwa vile wanamharibia maisha yake.
Muigizaji nyota wa filamu nchini, Wema Sepetu amewatimua watu wanaojiita Team Wema waliotapakaa katika mitandao mbalimbali ya kijamii, akisema hawataki kwa vile wanamharibia maisha yake.
Katika sauti aliyoituma katika akaunti ya mtandao wake wa Instagram,
alisema haelewi hasa asili ya watu hao kujihusisha na jina lake, lakini
anakerwa zaidi nao kwa kitendo chao cha kutaka kuingilia maisha yake
binafsi, ikiwa ni pamoja na kumshambulia mama yake.
Staa wa Bongo Movies, Wema Sepetu akiwa na aliyekuwa mpenzi wake mshindi wa BBA 2014, Idris Sultan.
“Siwajui hawa watu na sijui walikotokea, nasema siitaki hiyo team
Wema kwa sababu hainisaidii lolote, kama ni huyo Idriss endeleeni naye,
sitaki kusikia kabisa, hawana mchango wowote kwani, hao ni wanafiki na
mimi katika maisha yangu sitaki unafiki, mimi ni mtu wa wazi, sitaki,”
alisema msanii huyo.
Kukiwa na sauti zinazoonekana kumpunguza jazba mrembo huyo
aliyeshinda taji la Miss Tanzania mwaka 2006, Wema hakukubali, bali
aliendelea kutoa maneno makali akiwashutumu watu hao, ambao kwa muda
mrefu, wamejitambulisha kama mashabiki wake wanaopambana kwa nguvu kubwa
na wapinzani wake kisanaa.
Wema akiwa na mama yake, Mariam Sepetu.
(HABARI NA GLOBALPUBLISHERS.CO.TZ)
Post a Comment