THEO WALCOTT AONYESHA MAKALI YAKE NA KUIPA USHINDI ARSENAL
Theo Walcott ameonyesha makali yake
kwa kufunga magoli mawili wakati Arsenal ikiibuka na ushindi wa
magoli 2-0 dhidi ya Basel katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Iliwachukua washika mitutu dakika
sita kupata goli la kwanza kupitia Walcott akifunga kwa kichwa mpira
wa kona uliopigwa na Alexis Sanchez.
Wachezaji hao wawili wa Arsenal
walishirikiana tena na kutoa fursa kwa Walcott kufunga goli la pili
kwa shuti la chini.
Theo Walcott akifunga goli lake la kwanza kwa kichwa
Post a Comment