NDOA ZA UTOTONI ZINARUDISHA MAENDELEO YA WATOTO WA KIKE-WADAU WA KUTETEA HAKI ZA WATOTO.

 Mkurugenzi Mtendaji wa Kitua Sheria na Haki Binadamu, Dk.Hellen Kijo Bisimba akizungumza na waandishi wa habari leo katika mdahalo wa kupinga ndoa za utotoni iliyoandaliwa na Shirika la Serikali C-SEMA iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.
                                        Picha ya pamoja ya wadau wa kutetea haki za watoto.
Na Chalila Kibuda, Globu Jamii. 
WADAU wa kutetea haki za watoto wameiomba serikali kuangalia upya sheria ya ndoa mwaka 1971 ambayo inaruhusu mtoto wa kike kuolewa miaka 14 kwa idhini ya wazazi kutokana na sheria hiyo kupitwa na wakati na kufanya mtoto wa kike kukosa haki msingi ya kupata elimu ambayo ndio inaweza kubadlisha maisha mtoto na taifa likapata maendeleo.
 

Wadau hao wameyasema leo katika mdahalo wa kutetea kwa kuondokana na ndoa za utotoni  iliyoandaliwa na Shirika lisilo la Serikali la C-SEMA iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam, wamesema kuwa ndoa za utotoni zimefanya watoto wa kike kukosa elimu pamoja na kupoteza maisha wakati wa kujifungua kutokana viungo vyao kukosa utayari kubeba ujauzito. 

Akizungumza katika mdahalo huo Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha  Sheria na Haki za Binadamu, Dk. Hellen Kijo Bisimba amesema kuwa ndoa za utotoni sasa ifike mwisho ili kuwapa watoto wakike kufurahi maisha yao ya kupata na waweze kuleta mchango katika taifa. 

Amesema kuwa watoto wa kike wamekuwa wakiolewa  wanaume ambao hawawafahamu ambapo inamfanya mtoto wa kike kuwa na kidonda maisha yake ya duniani kuolewa na mtu asiyemjua hivyo wakati umefika wa kuondokana na ndoa  za utotoni ili kuweza kuwapa furaha ya maisha ya watoto wa kike.
 

Katika mdahalo huo mtoto  X  mkoani... ameeleza kuwa wazazi wake walichukua mahali kwa mwanaume ambaye hamujui lakini aliweza kutoroka ili asiolewe siku moja kabla harusi na kuweza kuhifadhiwa na taasisi na kuweza kuendelea na masomo kuanza kidato cha kwanza.
Mtoto X ametaka wadau wasaidie katika kuwasaidia watoto wa kike katika ndoa za utotoni kwani mateso makubwa wanayapata na wakati mwingine wanakuwa wanaolewa watu wasio wajua na wenye umri mkubwa kuanzia mika 50.
 

Aidha mtoto X  ametaka sheria ya mwaka 1971imekuwa ndio kimbilio ya wazazi kuozesha watoto katika umri mdogo na kufanya watoto wa kike kushindwa kufurahia maisha pamoja kukosa elimu ikiwa ni silaha ya mtoto wa kike.
Naw Mratibu wa C-sema, Michael Kehongoh amesema kuwa kampeni ya kumtetea mtoto wa  kike ni endelevu hivyo kunahitaji sauti moja ya katika kuokoa watoto hao.

No comments

Powered by Blogger.