Serikali Yakanusha Taarifa Inayosambazwa Katika Mitandao ya Kijamii Kwamba Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan Ameomba Kujiuzulu
Ofisi
ya Makamu wa Rais inakanusha taarifa inayosambazwa kwenye mitandao ya
kijamii kwamba Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama
Samia Suluhu Hassan, ameomba kujiuzulu nafasi yake na kwamba taarifa
hiyo ni ya uzushi na uongo haina ukweli wowote.
Taarifa
hiyo ni ya uchochezi inayolenga kuliweka Taifa kwenye taharuki. Mhe.
Makamu wa Rais yuko bega kwa bega na Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania katika kufanya kazi zao kwa mujibu wa Katiba ya nchi ili
kuwaletea wananchi maendeleo.
Ofisi
ya Makamu wa Rais inawataka wananchi na Watanzania kwa ujumla kupuuza
taarifa hiyo ambayo inalenga kupotosha umma kuhusu ushirikiano mzuri
uliopo baina ya Viongozi wetu.
Mwisho,
Ofisi ya Makamu wa Rais inawasihi Watanzania kufanya kazi kwa bidii na
wajiepushe na vitendo vinavyolenga kuvuruga amani na utulivu nchini.
Imetolewa na
Ofisi ya Makamu wa Rais
Dar es Salaam
Post a Comment