Polisi Washuhudia Majambazi Yakitwangana Risasi.......Zakamatwa Shehena za Silaha na Vifaa vya Uhalifu
WATU
watatu wanaosadikiwa kuwa ni majambazi wa kutumia silaha, ambao
wamehusika kufanya matukio mbalimbali ya kihalifu katika mkoa wa Dar es
Salaam, wameuawa na majambazi wenzao katika eneo la Vikindu wilaya ya
Mkuranga mkoani Pwani.
Licha
ya kuuawa kwa majambazi hao, Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es
Salaam, limefanikiwa kuwakamatwa watu zaidi ya saba, wanaosadikiwa
kuhusika na tukio la majibizano ya risasi na polisi, lililotokeo Vikindu
lililosababisha kifo cha askari mmoja.
Akizungumza
na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Kamishna wa Polisi
Kanda Maalumu, Simon Sirro alisema kabla ya kuuawa watuhumiwa hao
walikamatwa katika maeneo tofauti ya Mbagala, Keko na Kawe jijini humo.
Alisema
watu hao walikamatwa kufuatia tukio la ujambazi, lililotokea Agosti 29,
mwaka huu katika Jengo la Sophia House maeneo ya Veta Changombe, ambapo
majambazi hao walidaiwa kupora Sh milioni 35 na kutoweka kwa kutumia
gari aina ya Toyota Noah lenye namba bandia T 549 BPK
.Aliongeza kuwa uchunguzi wa tukio hilo, uliendelea kufanyika na Septemba 3, timu ya upelelezi kutoka Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, iliweka mtego na kufanikiwa kuwakamata majambazi hao watatu na walipohojiwa walikiri kufanya matukio mbalimbali ya ujambazi wa kutumia silaha na kuweza kutaja silaha mbalimbali walizonazo.
.Aliongeza kuwa uchunguzi wa tukio hilo, uliendelea kufanyika na Septemba 3, timu ya upelelezi kutoka Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, iliweka mtego na kufanikiwa kuwakamata majambazi hao watatu na walipohojiwa walikiri kufanya matukio mbalimbali ya ujambazi wa kutumia silaha na kuweza kutaja silaha mbalimbali walizonazo.
Kamanda
Sirro alisema majambazi hao, waliwapeleka askari eneo la Mbezi Chini
katika nyumba waliyokuwa wamekodi na askari walifanya upekuzi na
walifanikiwa kupata silaha mbalimbali, zikiwemo bunduki 23 na risasi
zaidi ya 800 na vitu vinginevyo.
Alitaja
silaha hizo kuwa ni bunduki za kijeshi tatu aina ya SMG zikiwa na
magazini nane na risasi 120, bastola 16, magazini tatu za bastola na
risasi moja, Shot gun pump action tatu na risasi 130, bastola 16
magazini na risasi 548 na bunduki tatu aina ya Shot gun na risasi zake
130.
Aidha
alisema walikuta redio za mawasiliano 12 na chaja zake tatu, darubini
za kuonea mbali tatu, pingu za plastiki 45, majaketi ya kuzuia risasi
matatu, mkasi mmoja wa kukatia vyuma, mtarimbo mmoja, risasi baridi za
kutishia 37, boksi moja la kusafishia silaha, nyundo kubwa moja, pingu
za chuma tatu, mashine moja ya kuhifadhia kumbukumbu na magari mawili.
Alisema
uchunguzi wao ulibaini kuwa majambazi hao Septemba 6, mwaka huu
walipora bunduki aina ya Shot gun yenye namba 006091830, ikiwa na risasi
moja katika barabara ya Mbozi Chang’ombe.
Sambamaba
na hayo, majambazi hao walikiri kuhusika na wizi wa mamilioni ya fedha
katika Benki ya Habib African ya Kariakoo mwaka 2014 na Benki ya Stanbic
mwaka 2014, wakitumia gari aina ya Toyota Noah.
Kamanda
Sirro alisema baada ya mahojiano zaidi, majambazi hao walisema wanazo
silaha nyingine ambazo wamezificha Vikindu wilaya ya Mkuranga mkoani
Pwani. Ndipo askari walifuatana na watuhumiwa hao hadi kwenye msitu wa
Vikindu.
Alisema
askari walipofika eneo hilo, walilodai ni karibu na zilipo silaha hizo,
walishuka kwenye gari na kuingia porini wakiwa wamewatanguliza
watuhumiwa mbele majira ya usiku.
Aliongeza
kuwa wakiwa msituni humo na askari wakiwa wenye tahadhari kubwa, ghafla
walisikia milio ya risasi ikitokea mbele, ambapo askari walilala chini
na baadaye zikisikika sauti zikisema ‘mmetuua sisi’.
Alisema
baada ya risasi za mfululizo kutulia, askari walishuhudia majambazi hao
ambao walichelewa kulala chini wakati risasi zikipigwa wakiwa
wamejeruhiwa sehemu za kifuani na tumboni huku wakivuja damu nyingi.
Alisema
askari walipiga risasi kuelekeza eneo zilikotokea risasi na
walipoendelea kusonga mbele, walikuta silaha aina ya SMG ikiwa
imetelekezwa na haikuwa na risasi ndani ya magazine, hivyo kufanya idadi
ya silaha za SMG kufikia nne.
Aidha
alisema askari waliwabeba majambazi hao na kuwapeleka kwenye gari
kuelekea hospitalini, lakini wote walifariki dunia wakiwa njiani
kutokana na kutoka damu nyingi.
Akizungumzia
tukio la Vikindu, Sirro alisema wamefanikiwa kuwakamata watu hao
wanaosadikiwa kuhusika na tukio ambalo lilisababisha kifo cha askari
mmoja.
“Majambazi
hao walikuwa ni kundi la kama watu 14 na tayari tumewakamata zaidi ya
saba ambao mpaka sasa tunawashikilia kwa mahojiano zaidi ili kufanikisha
upelelezi,” alisema Kamanda Sirro.
Pia
alisema kumekuwa na taarifa mbalimbali, zikisambazwa katika vyombo vya
habari zikidai kuwa katika tukio la Vikindu, kuna askari anahusika na
tukio hilo na kudai taarifa hizo si za kweli na hakuna askari
aliyehusika katika tukio hilo.
Katika
tukio lingine, jeshi hilo limefanikiwa kuwakamata watuhumiwa wanne kwa
makosa ya wizi wa magari manane, likiwemo gari moja la kibalozi.
Kamanda
Sirro alisema magari hayo yaliibwa jijini Dar es Salaam na kuuzwa kwa
watu mbalimbali jijini hapo na mikoani na watuhumiwa wote wanaendelea
kuhojiwa na mara upelelezi utakapokamilika watapelekwa mahakamani kujibu
tuhuma zinazowakabili.
Sirro
alisema katika tukio lingine jeshi hilo limefanikiwa kuwakamata
watuhumiwa sita wanaodaiwa kuhusika na kuvunja nyumba usiku na kuiba.
Post a Comment