Picha: Shuhudia Nyumba Mpya Za Yamoto Band
Nyumba mpya watakazomiliki wasanii wa Yamoto Band.
Akizungumza na mtandao huu mara baada ya kuzitambulisha nyumba hizo, Fella alisema kuwa kila mmoja atakabidhiwa hatimiliki yake na kwamba ni nyumba zinazojitegemea.
“Kama uonavyo, nyumba zipo nne kwa Yamoto ambazo zote zinafanana hadi ndani. Ukiingia kuna master, vyumba viwili. Eneo la kulia chakula, jiko na sebule kubwa,” alisema Fella.
Aidha, Fella ameelekeza shukrani zake kwa Rais Mstaafu Jakaya Kikwete kwa kumpa hamasa na kufanikisha zoezi zima la kujenga nyumba hizo.
“Nawashukuru wote japo siwezi kumshukuru mmojammoja. Shukran za pekee nizielekeze kwa Rais Kikwete kwa kutoa hamasa sana kwa vijana hawa wa Yamoto. Ruge naye nime shukran kwa kuweza kuiinua Yamoto kwani nakumbuka baada ya bendi hii kuanza kusimama kuna kipindi tulikwama vifaa lakini Ruge kupitia bendi yake kipindi kile ya Odama Band walitusaidia na hata Asha Baraka naye anamchango mkubwa katika bendi hii ya Yamoto,” aliongeza Fella.
Fella alimalizia kwa kusema kuwa, nyumba hizo zimetokana na jasho la Yamoto kupitia shoo zao na milio ya simu ambayo imefanikisha.
“Pia kuna nyumba ambayo ipo katika hatua ya mwisho kukamilia, iko pembeni ya nyumba za Yamoto. Ni nyumba ya mshindi wa shindano la Bongo Star Search, Kayumba.”
Yamoto inaundwa na wasanii wanne, Enock Bella, Maromboso, Dogo Aslay na Beka One.
Yamoto imetoka kwenye familia ya Mkubwa na Wanawe ambayo kwa sasa ina takribani wasanii 102 wanaosomeshwa na kuimba muziki.
Credit: Andrew Carlos/GPL
Mkurugenzi wa Mkubwa na Wanawe ambaye
pia ni mmiliki wa Yamoto Band, Said Fella akiongea na wanahabari wakati
akitambulisha nyumba mpya watakazomiliki Yamoto Band. Kulia ni Asha
Baraka.
LEO mchana, Mkurugenzi wa Mkubwa na Wanawe ambaye pia ni mmiliki wa
Yamoto Band, Said Fella alitambulisha kwa waandishi nyumba mpya
wanatakazomiliki bendi yake hiyo zilizopo Mbande-Kisewe jijini Dar.Akizungumza na mtandao huu mara baada ya kuzitambulisha nyumba hizo, Fella alisema kuwa kila mmoja atakabidhiwa hatimiliki yake na kwamba ni nyumba zinazojitegemea.

Post a Comment