MABADILIKO MENGINE LIGI KUU BARA, SASA MECHI KUCHEZWA SIKU 3 MFULULIZO
Ligi
Kuu ya Vodacom Tanzania Bara inatarajiwa kuendelea kesho Jumamosi na
Jumapili kwa michezo mitano ya mzunguko wa nne lakini kuna mabadiliko
yamefanyika ambapo sasa Jumatatu pia kutakuwa na mchezo wa ligi hiyo.Shirikisho
la Soka Tanzania (TFF) limefanya mabadiliko hayo katika mchezo wa
African Lyon na Mbao FC uliokuwa uchezwe kesho Jumamosi, sasa ndiyo
ambao utachezwa Jumatatu Septemba 12, 2016.
Mabadiliko hayo ni mwendelezo wa mabadiliko kadhaa ya ligi hiyo ambayo imeanza hivi karibuni. Mchezo huo utafanyika kwenye Uwanja wa Uhuru baada ya African Lyon kubadili uwanja kutoka Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume. Michezo
ya Jumamosi mingine itaendelea kama kawaida ukiwemo ule wa wapinzani wa
jadi kati ya JKT Ruvu itakayokaribishwa na Ruvu Shooting kwenye Uwanja
wa Mabatini ulioko Mlandizi mkoani Pwani wakati Mwadui FC itakuwa
mwenyeji wa Stand United kwenye Uwanja wa Mwadui Complex, Shinyanga. Mbali
ya michezo hiyo, pia Yanga itakuwa mwenyeji wa Majimaji ya Songea
kwenye Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam, wakati Azam FC ambayo itakuwa
mgeni tena kwenye Uwanja wa Sokoine ikicheza na Mbeya City na kwenye
Uwanja wa Nangwanda Sijaona Ndanda itaikaribisha Kagera Sugar ya Kagera. Ligi
hiyo itaendelea Jumapili, Septemba 11, 2016 kwa Simba kuikaribisha
Mtibwa Sugar ya Morogoro kwenye Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam.
Post a Comment