KATIBU MKUU OFISI YA WAZIRI MKUU AFANYA ZIARA KATIKA VIZUIZI VYA BARABARANI (MIZANI)
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu) Dkt. Hamisi
Mwinyimvua akiweka sahihi katika kitabu cha wageni wakati wa ziara yake
katika Vizuizi vya barabarani (Mizani) na Mipakani kwa lengo la kufanya
Tathimini ya Utekelezaji wa mpango wa maboresho ya mazingira ya biashara
na uwekezaji nchini Septemba 15, 2016.
Msimamizi wa Kituo cha Mamlaka ya Mapato TRA kilichopo Mkoani
Pwani Bw. David Kisanga akitoa maelezo juu ya utendaji wa ofisi zao kwa
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu) Dkt. Hamisi
Mwinyimvua wakati alipotembelea ofisi hizo Mkoa wa Pwani.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu) Dkt. Hamisi
Mwinyimvua akimsikiliza Msimamizi wa Kizuizi cha Vigwaza Mkoani Pwani
Bw. Titus Michael wakati wa ziara yake kujionea hali halisi ya vituo
hivyo kwaajili ya Maboresho ya mazingira ya biashara na Uwekezaji
nchini.
Baadhi ya magari yakipima uzito wa mizigo katika Mizani ya Vigwaza
mkoa wa Pwani, Septemba 15, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Post a Comment