GARETH BALE, CRISTIANO RONALDO WAPO TAYARI KUIVAA BORUSSIA DORTMUND
Kocha Zinedine Zidane ameendelea
kuangali kikosi chake cha Real Madrid kikijiandaa kwa mchezo wao wa
leo wa Ligi ya Mabingwa dhidi ya Borussia Dortmund.
Gareth Bale, Cristiano Ronaldo
pamoja na wachezaji wengine wameonekana wakiwa katika ari ya kuibuka
na ushindi katika mchezo huo wa leo usiku.
Aidha, Zidane amekanusha kuwapo kwa
mgogoro wowote baina yake na Ronaldo, ambao ulivumishwa baada ya
kocha huyo kumtoa Ronaldo kabla ya mchezo kuisha mwishoni mwa wiki.
Cristiano Ronaldo akijifua na wachezaji wenzake
Post a Comment