Yaliyoafikiwa Kwenye Mkutano wa Dharula wa Yanga Kuhusu Mzee Akilimali
Mbali na viongozi kadhaa wa matawi,
mashabiki wengi walionekana wakizunguka eneo la klabuni hapo kutaka
kujua nini kinachoendelea na kama ni kweli Manji kaamua kujiuzulu au la,
lakini hakukuwa na tamko la ziada tofauti na kile kilichoandikwa na
mtandao huu kuwa Manji bado hajatoa tamko rasmi.
Mmoja kati ya viongozi wa matawi ya
Yanga mkoa wa Dar es Salaam anayeiwakilisha Kanda ya Temeke, Robert
Liungu, ametaja maazimio waliyofikia kutoka katika mkutano huo wa
dharura.
Kwanza kabisa, wanachama wa Yanga wanatambua kuwa Manji bado ni Mwenyekiti wao kwa mujibu wa katiba yao.
Pili, wanachama wamemuomba mdhamini mzee
Katunda amtoe Akilimali katika nafasi ya katibu wa wazee wa Yanga kwani
ndiye anayedaiwa kumpinga Manji.
Tatu, wanachama wanaiomba Kamati ya
Utendaji ya Yanga imuite Akilimali imuhoji na kumsimamisha uanachama kwa
madai kuwa yeye ni Simba.
Nne, wanachama wa matawi yote wanaendelea kumtambua Yusuph Manji kama Mwenyekiti wao, alizungumza Robert Liungu.
Post a Comment