TAARIFA ZA MANJI KUACHIA NGAZI, MZEE AKILIMALI ASEMA AMEITWA KUYAMALIZA
Wakati sekeseke la Mwenyekiti wa Yanga,
Yusuf Manji kudaiwa kujiuzulu nafasi yake hiyo, mwanachama mkongwe wa klabu
hiyo, Ibrahim Omary Akilimali maarufu kwa jina la Mzee Akilimali ametoa kauli tata juu ya sakata
hilo.Wakati huu ambapo
Manji hatatoa tamko lolote juu ya uamuzi wake huo wa kujiuzulu, Mzee Akilimali
amenukuliwa akisema kuwa kuna watu wa Yanga wamemuita ili kuzungumza kuumaliza
mvutano unaoendelea ambapo inaelezwa kuwa mzee huyo amechangia maamuzi ya Manji
kujiondoa Yanga kutokana na kumshutumu kwa maneno mengi.
Akihojiwa na
kituo cha Radio ha EFM, muda mfupi uliopita Mzee Kilimali alinukuliwa akisema: “Msitake
kuyakuza haya mambo, subirini kwanza nataka tuyamalize, mimi wameniita ndiyo maana
nipo huku ili kuyamaliza.”
Alipoulizwa yupo
wapi na ameitwa na nani, Akilimali alisema: “Nimekwambia nimeitwa huku, wewe
subiri kwanza tuyamalize kisha utanipigia, subiri baada ya nusu saa nitakubeep
unipigie.”
Licha ya
kuendelea kubanwa kufafanua zaidi juu ya kinachoendelea, mzee huyo alisisitiza
kuwa pigiwe baadaye na kukata simu.
Mzee Akilimali ni
mzaliwa wa Kigoma, ambapo anadai alianza kuipenda Yanga tangu miaka ya 1950.
Post a Comment