WEMA ADAIWA KUMTELEKEZA MIRROR! Baada ya kupata ajali na kuvunjika mguu…


 Baada ya kupata ajali ya gari kisha kuvunjika mfupa wa paja la mguu wa kushoto, msanii wa Bongo Fleva ambaye aliwahi kuwa chini ya usimamizi wa staa wa sinema za Kibongo, Wema Isaac Sepetu, Miraj Juma ‘Mirror’ anadai kutelekezwa na mrembo huyo akiwa hospitalini. Mirror ameliambia Ijumaa
kuwa alipata ajali hiyo hivi karibuni akiwa na gari la Wema aina ya Toyota Crown, maeneo ya Mbezi-Beach  jijini Dar akitokea Ledger Hotel kufanya mazoezi.
Mirror ambaye amelazwa kwenye Hospitali ya Rabininsia Memorial iliyopo Tegeta, Dar alisema alipata ajali hiyo wakati akimkwepa mama aliyekuwa na mtoto. Alisema kuwa, baada ya ajali hiyo alipoteza fahamu hadi
alipozinduka na kujikuta hospitalini hapo hivyo akawa akifanya mawasiliano na Wema kumwelezea hali yake lakini mrembo huyo hakufika kumjulia hali.Mmoja wa ndugu aliyekuwepo hospitalini hapo ambaye hakupenda kutaja jina lake alisema kuwa, walau Wema angefika kumchangia Mirror fedha za
matibabu kwani anadaiwa zaidi ya Sh. milioni 1.3 ili afanyiwe operesheni. Hata hivyo, baadaye Wema aliahidi kufika lakini hakutokea hadi gazeti hili linaondoka hospitalini hapo. Ijumaa lilimtafuta Wema
bila mafanikio kufuatia simu yake kuita bila kupokelewa na hata alipotumiwa SMS hakujibu huku watu wake wa karibu wakisema kuwa yupo mikoani kwa ajili ya projekti yake mpya ya kuandaa shoo za vigoma.
Jitihada za kumpata bado zinaendelea

No comments

Powered by Blogger.