Polisi mkikuta mtu kwenye msitu piga, haki za binadamu waje kwangu’ -RC Makonda
August 25
2016 baadhi ya viongozi wa Serikali akiwemo Waziri wa mambo ya ndani ya
nchi Mwigulu Nchemba, Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda
wameungana na watanzania wengine kuaga miili ya Askari Polisi
waliofariki kwa kupigwa risasi katika shambulio lililotokea Mbande, Dar
es salaaam usiku wa August 23 2016.
Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam ni miongoni mwa viongozi waliosimama kuongea ambapo amesema…>>>’Hatujapata taarifa kwamba majambazi waliohusika wanatoka nchi nyingine maanayake ni ndugu zetu wanaoishi kwenye majumba yetu‘ –RC Makonda
‘Askari
mmoja analinda watu zaidi ya 500 kwamaana hiyo kupoteza askari wanne
maana yake wananchi wasiopungua 6000 wanakaa bila ulinzi, natoa wito kwa
wanaojiita haki za binadamu‘ –RC Makonda
‘Askari
ukikutana na mtu yoyote kwenye msitu wewe pinga alafu hao haki za
binadamu waje kwangu, hatuwezi kuishi kwenye mkoa kama huu wakati Askari
wetu tunawaondoa na natoa wito kama kuna haki za binadamu basi nataka
haki za askari wangu kwanza‘ –RC Makonda
Post a Comment