Miili ya askari waliouawa mbagala yaagwa

WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba ameongoza mamia ya waombolezaji wakiwemo viongozi wa Serikali, Makamishna wa Polisi na wakazi wa Dar es Salaam kuaga miili ya Askari Polisi watatu kati ya wanne waliouawa katika shambulio la ujambazi.
Askari hao waliuawa Jumanne usiku katika eneo la Benki ya CRDB, Mbande, Kata ya Chamanzi, Wilaya ya Temeke Jijini Dar es Salaam baada ya watu wenye silaha kuwavamia wakiwa kazini na kupora bunduki mbili aina ya SMG na risasi 60.
Miili ya askari iliyoagwa katika viwanja vya Polisi Barabara ya Kilwa ni ya Koplo Yahaya Malima aliyesafirishwa kwenda kuzikwa kijiji cha Kibuta, Wilaya ya Kisarawe Mkoani Pwani, Tito Mapunda aliyesafirishwa kwenda Kijiji cha Migoli, Wilaya ya Iringa vijijini mkoani Iringa na Gaston Lupanga aliyesafirishwa kwenda mjini Songea mkoani Ruvuma kwa maziko.
Askari mwingine Koplo Khatib Ame Pandu alisafirishwa kwenda Zanzibar ambapo maziko yalifanyika siku hiyo hiyo.
Mbali na Waziri Mwigulu, viongozi wengine wa serikali waliotoa heshima za mwisho kwa miili ya marehemu ni Waziri wa Katiba na Sheria, Dk Harison Mwakyembe, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, George Masaju, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Hamad Masauni na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira.
Viongozi wengine ni Mkuu wa Jeshi la Polisi, Ernest Mangu, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Felix Lyaniva, Meya wa Manispaa ya Temeke, Abdallah Chaurembo,Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) Biswalo Mganga na Mkuu wa Makosa ya Jinai, DCI, Diwani Athuman

No comments

Powered by Blogger.