Polisi Yapeleka Askari wengine 80 Kuongeza nguvu Katika Oparesheni Ya Kusaka Majambazi Huko Vikindu, Mkuranga
Jeshi
la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limeongeza nguvu kwa kutuma
askari wengine 80 katika oparesheni ya kusaka majambazi inayoendelea
katika maeneo ya Vikindu, wilayani Mkuranga mkoani Pwani.
Akizungumza na vyombo vya habari leo katika kituo kikuu cha Polisi Dar es Salaam, Kamanda wa Polisi wa kanda hiyo Kamishna Simon Sirro, amesema Jeshi hilo limeanza rasmi oparesheni hiyo usiku wa kuamkia jana, ikiwa na lengo la kusaka watu wanaoshukiwa kuwa ni majambazi wanaodaiwa kufanya matukio kadhaa ya ujambazi likiwemo lile la kuuawa kwa askari wanne waliokuwa wakienda lindoni, katika benk ya CRDB, Mbande jiji Dar es Salaam.
Amesema
kuwa katika oparesheni hiyo kuna watu waliouawa na wengine
wanashikiliwa na jeshi hilo, lakini amekataa kutaja idadi yoyote ile ya
waliouawa au waliokamatwa kwa sababu za kiusalama kwa kuwa oparesheni
hiyo bado inaendelea.
Usiku wa kuamkia jana, hali ya taharuki iliwakumba wakazi wa Vikindu baada ya kikosi maalum cha askari kuvamia nyumba moja iliyoko eneo hilo, na kisha kuzuka kwa majibizano ya risasi kati ya polisi na wanaodaiwa kuwa ni majambazi waliokuwa katika nyumba hiyo.
Baadhi ya askari wakiwa tayari kwenye magari yao wakati wa kujiandaa kuelekea Vikindu kwenye mapambano
Akizungumza na vyombo vya habari leo katika kituo kikuu cha Polisi Dar es Salaam, Kamanda wa Polisi wa kanda hiyo Kamishna Simon Sirro, amesema Jeshi hilo limeanza rasmi oparesheni hiyo usiku wa kuamkia jana, ikiwa na lengo la kusaka watu wanaoshukiwa kuwa ni majambazi wanaodaiwa kufanya matukio kadhaa ya ujambazi likiwemo lile la kuuawa kwa askari wanne waliokuwa wakienda lindoni, katika benk ya CRDB, Mbande jiji Dar es Salaam.
“Itakuwa
ni kinyume cha utaratibu nikieleza kinachoendelea kwenye operesheni,
niwahakikishie silaha zilizochukuliwa zinarudi,kinachoendelea
nitawajulisha jumanne ili wananchi wajue kitu gani kinaendelea,” amesema.
Ameongeza kuwa; “Mapambano ni ya kawaida sana, na ndio maana askari
polisi akifa kwa silaha ni jambo la kawaida sana. Operesheni tutaifanya
maeneo ya Vikindu, Pwani Dar es Salaam, sababu hii network (mtandao)
ipo na lazima tutaisafisha.Kama walidhani wataitawala DSM wamejidanyanya lazima tutarudisha heshima ya jiji.”
Katika
hatua nyingine, Sirro amesema amepata taarifa kuwa wapo baadhi ya watu
wanapewa fedha kwa ajili ya kufanya maandamano Septemba Mosi mwaka huu
ambapo ametoa onyo kwa watakaoshiriki kuwa watachukuliwa hatua kali za
kisheria kwa kuwa maandamano hayo hayajaruhusiwa.
“Wote tunajua madhara ya fujo, wazalendo naomba msishiriki, Wanaotaka kujionesha wanapambana na polisi waje barabarani, ” amesema.
Vikosi hivyo vikitoka makao makuu ya kanda maalum ya Dar kuelekea kwenye mapambanoUsiku wa kuamkia jana, hali ya taharuki iliwakumba wakazi wa Vikindu baada ya kikosi maalum cha askari kuvamia nyumba moja iliyoko eneo hilo, na kisha kuzuka kwa majibizano ya risasi kati ya polisi na wanaodaiwa kuwa ni majambazi waliokuwa katika nyumba hiyo.
Baadhi ya askari wakiwa tayari kwenye magari yao wakati wa kujiandaa kuelekea Vikindu kwenye mapambano
Post a Comment