NDEGE YA EMIRATES IKIWA NA WATU 300 YAWAKA MOTO WAKATI IKITUA
Dubai Ndege ya Shirika la
Ndege la Emirates iliyokuwa ikijiandaa kutua katika Uwanja wa Kimataifa
wa Dubai imewaka moto na kusababisha
taharuki kubwa kwa abiria waliokuwamo kwenye ndege hiyo.
Ndege hiyo Boeing 777-300 ilikuwa na abiria 282 na
wafanyakazi 18 na hakuna aliyejeruhiwa. Abiria wote waliokolewa kupitia mlango
wa dharura wa ndege hiyo iliyouwa ikiruka kutoka Trivandrum, India.
Waliondolewa kwenye eneo la tukio ndani ya dakika 45 tangu
kwa ndege hiyo kuwaka moto huku vyombo vya zimamoto zikichukua hatua ya haraka
kuudhibiti moto huo.
Ndege hiyo iliwaka moto muda mfupi baada ya kutua kwenye
uwanja huo na kwamba hadi sasa hakuna taarifa za kile kilichobabisha kuzuka kwa
moto huo.
Miongoni mwa abiria waliokuwemo kwenye ndege hiyo ni pamoja
na 24 Wabritons, sita Wamarekani, wanne Waireland na wawili Waustralia.
Post a Comment