RAIS AMTEUA MKEWE KUWA MGOMBEA MWENZA WA URAIS
Rais wa Nicaragua, Daniel Ortega (70) amemteua mkewe kuwa mgombea
mwenza nafasi ya makamu wa rais wakati huu ambapo anawania kuchaguliwa kwa
muhula mwingine.
Mkewe Rosario Murillo tayari ana wadhifa maarufu wa msemaji
wa serikali, amekuwa akionekana katika runinga ya Nicaragua kila siku na
anaonekana kuwa anagawana mamlaka na mumewe.
Wakosoaji wanawashtumu wanandoa hao wawili kwa kuiendesha
Nicaragua ambayo inakabiliwa na uchaguzi mkuu mwezi Novemba kama chombo chao
cha kibinafsi. Rais Ortega akiwa hazungumzi sana katika vyombo vya habari
,mkewe huonekana mara kwa mara katika runinga akijadili sera na kujikuza .
Akiwa mama wa watoto 7 wa rais huyo anajua kuongea
Kiingereza na Kifaransa huku akijulikana pia kuwa mshairi. Pia anasifa za kuvaa
mavazi yenye rangi nyingi na vito vya miaka ya sitini.
Wanahabari wanasema kuwa raia wengi wa taifa hilo wanamuona
bi Murillo kama mwenye uwezo mkubwa katika taifa lake kutokana na hadhi yake
katika uma.
Mume na mkewe waliwasilisha makaratasi yao ya kugombea viti
hivyo rasmi katika mji mkuu wa Managua wakiandamana na mshauri wakili wa chama
chao cha Sandinista.
Post a Comment