Basi la kisasa zaidi lazinduliwa China
MAFANIKIO ya Kiteknolojia yanazidi kupiga
hatua sehemu mbalimbali duniani! Hii ni baada ya nchi ya China kuzingua basi la
kipekee maarufu kama Transit Elevated Bus (TEB) lenye urefu wa mita mbili juu
linaloruhusu magari ya kibinafsi kupitia uvunguni mwake limefanyiwa majaribio
katika mji wa Hebei, Kaskazini mwa nchi hiyo.
Basi hilo linalotumia umeme pia lina urefu wa
mita 21 na upana wa futi 25, linategemewa kutatua tatizo la usafirishaji
wa abiria katika miji yenye idadi kubwa ya watu, lina uwezo wa kubeba zaidi ya
watu 300 .
Hii ndio mara ya kwanza kwa wabunifu kuonesha
basi hilo hadharani baada ya video yake kuonekana katika mitandao ya kijamii
mwezi Mei.
Tathimini iliyofanywa na watengenezaji wa basi
hilo imeeleza kuwa, basi moja la TEB lina uwezo wa kubeba abiria wote katika
mabasi 8 ya kawaida na linauwezo wa kuhudumu kwa kasi ya Kilomita 60 kwa saa na
likiwa kwenye safai zake, gari zingine ndogo ndogo zinaweza kupita chini ya
basi hilo bila kuleta madhara.
Takriban mabasi hayo manne yanaweza
kuunganishwa na hivyo kuwa na dereva mmoja.
Hivi ndivyo inavyoonekana
”Mabasi haya ni ya kipekee na moja ya faida
yake kuu ni uwezo wake wa kubeba abiria wengi sana 300 kwa kila basi, pia
itaokoa sana nafasi barabarani” alisema mhandisi mkuu katika mradi huo mpya wa
usafiri Song Youzhou.
”Inahudumu kama vile treni za kisasa za umeme
ila gharama ya kuwekeza kujenga njia na ukarabati barabarani ikiwemo ujenzi wa
vituo maalum vya TEB.
Post a Comment