MCHUNGAJI AFARIKI KWA KUFUNGA SIKU 30 AKIJARIBU KUVUNJA REKODI YA YESU
LILE andiko la usimjaribu bwana Mungu wako lililosemwa na
Yesu Kristu limejidhihirisha baada ya mchungaji maarufu nchini Afrika Kusini,
Alfred Ndlovu (44), kufariki dunia baada ya kufunga usiku na mchana kwa
takribani siku 30 akitaka kuvunja rekodi ya Yesu Kristu aliyefunga siku 40 bila
kula kitu chochote.
Kama alivyofanya Yesu Kristu, Mchungaji Ndlovu naye
aliondoka nyumbani kwake Juni 17 mwaka
huu na kuelekea nyikani kwa ajili ya kufunga na kuomba, huku akiweka pembeni
anasa za dunia.
Kifo cha mchungaji huyo kimeishangaza sana familia yake,
waumini wa kanisa lake na jamii nzima kwa ujumla.
Mchungaji huyo alijulikana kwa imani yake thabiti
ambayo ingeweza hata kuhamisha milima.
Mmoja wa wanafamilia ya mchungaji huyo alisikika
akilalamika; “Alikuwa mtu wa imani sana. Lakini kwa bahati mbaya amefariki kifo
hicho. Baada ya mwezi ndipo tumepata taarifa za kifo chake”
Akijaribu kuvunja rekodi ya Yesu, Mchungaji Ndlovu alifariki
baada ya kufunga kwa takribani siku 30 japokuwa hakuwahi kuripotiwa kuwa na ugonjwa
wowote hapo awali. Alikuwa peke yake nyikani na maiti yake iligunduliwa na
mpita njia mmoja aliyetoa taarifa polisi.
Post a Comment