BREAKING NYUZZZ...: KAIMU MKURUGENZI MKUU WA SHIRIKA LA NDEGE TANZANIA ASIMAMISHWA KAZI KWA UZEMBE
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof.Makame Mbarawa
amemsimamisha kazi Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Ndege Tanzania
(ATCL), Captain Johnson Mfinanga na Mkurugenzi wa Uendeshaji, Captain
Sadick Muze kwa kosa la kuchagua rubani mmoja ambaye hajakidhi vigezo
anavyotakiwa kuwa navyo marubani wanaotarajia kuondoka kesho
kuelekea nchini Canada kwa ajili ya mafunzo ya kurusha ndege mpya
mbili zinazotarajiwa kuwasili nchini katikati ya mwezi Septemba. Akizungumza
na waandishi wa habari wilayani Kyela, Mkoani Mbeya Prof. Mbarawa
amesema baada ya kukamilisha malipo ya awali ya ununuzi wa ndege mbili
mpya kwa ajili ya ATCL alitoa maelekezo kwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu huyo
kuwachagua marubani watano wenye vigezo ambavyo vinahitajika kwa ajili
ya mafunzo hayo jambo ambalo amebaini mmojawapo wa waliochaguliwa
hajatimiza vigezo na hivyo kuamua kumsimamisha kazi kwa kosa la uzembe.
Waziri Mbarawa amesisitiza kuwa msimamo wa serikali ni kuhakikisha kila mtumishi wa umma anatekeleza wajibu wake kwa kufuata sheria kanuni na taratibu hivyo atakaye kiuka msimamo huo Serikali haitasita kumchukulia hatua za kinidhamu.
Shirika la Ndege Tanzania katika mwaka huu wa fedha Serikali imetenga kiasi cha shilingi bilioni 500 kwa ajili ya ununuzi wa ndege tatu.

Post a Comment