Breaking News: Rais Magufuli Atengua Uteuzi Wa Mkuu Wa Mkoa Arusha Felix Ntibenda,amteua Mrisho Gambo Kuwa Mkuu Wa Mkoa
Mkuu Mpya wa Mkoa wa Arusha, Bw. Mrisho Gambo
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amefanya mabadiliko madogo ya uongozi
wake na kumteua Bw. Mrisho Gambo kuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha kuanzia
leo (Alhamisi, Agosti 18,2016).
Uteuzi wa Gambo unakuja takriban miezi miwili baada ya kuteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Arusha mwisho mwa Juni mwaka huu.
Felix Ntibenda, Mkuu wa Mkoa wa Arusha aliyetenguliwa.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema Bw.
Gambo anachukua nafasi ya aliyekuwa Mkuu wa Mkoa huo, Bw. Felix Kijiko
Ntibenda ambaye uteuzi wake umetenguliwa.
Amesema Bw. Ntibenda anahamishiwa Ofisi ya Waziri Mkuu ambako atapangiwa majukumu mengine.
Kabla ya uteuzi huo, Bw. Gambo alikuwa
Mkuu wa Wilaya ya Arusha. Ataapishwa kesho (Ijumaa, Agosti 19, 2016) saa
3 asubuhi Ikulu jijini Dar es Salaam.
Post a Comment