VANESSA AFUNGUKIA BATA WALIZOKULA SINGITA
Na Hamida Hassan
Wanamuziki, Vanessa Mdee na mpenzi wake Juma Jux ‘Jux’ baada
ya manenomaneno kuzagaa kuwa wameachana juzikati wapenzi hao walionekana kwenye
mbuga ya wanyama ya Serengeti iliyopo mkoani Mara kisha kwenda kula bata kwenye
hoteli ya bei mbaya ya Singita.
Akipiga stori na safu hii juzi akiwa Serengeti, Vanessa
alisema kuwa, wameamua kwenda huko kwa mapumziko ya siku nne ikiwa ni sehemu ya
kufanya utalii wa ndani na wamekula bata za kutosha.
“Ni mambo ya utalii wa ndani, tumekuja huku kupumzika
kidogo, siyo lazima kwenda nchi za nje kwa mapumziko, humuhumu Bongo kuna
sehemu unakwenda na unajisikia furaha,” alisema mwanadada huyo.
Singita ni hoteli ya kifahari iliyopo mkoani
Mara ambayo inaiingizia nchi fedha nyingi za kigeni.
Post a Comment