FAIZA, WEMA NDANI YA BIFU NZITO
faiza ali
IMELDA MTEMA, IJUMAA
MTIFUANO wa maneno makali umeibuka kati ya wasanii wa fi
lamu Bongo, Wema Sepetu na Faiza Ali chanzo kikiwa ni Faiza kuposti maneno ya
‘kumdis’ Wema kutokana na mfumo wake wa maisha ya kimapenzi.
Wema na Idris.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram Faiza aliandika kuwa Wema
anapenda sana ‘ving’asti’ (dogodogo) akitolea mfano Idris Sultan aliyekuwa
mpenzi wake, kisha akasema kuwa anaomba Mungu asije akapata mtoto wa kiume
atakayependa ku-date na wanawake waliomzidi umri.
Kutokana na maneno hayo yaliyojaa shari ndani yake, Ijumaa
lilimtafuta Wema kuzungumzia posti hiyo ambapo alipopatikana alikuwa na haya ya
kusema: “Yaani mimi simpendi kabisa yule binti, namuona ni mpumba** tu, ndiyo
maana hata Sugu akaona si mwanamke anayefaa kuwa mkewe. Hana akili kabisa.”
Post a Comment