MWANAMUZIKI KOFFI OLOMIDE AACHIWA HURU KUTOKA JELA BAADA YA KUTUMIKIA KIFUNGO KWA SIKU 2
Koffi
Olomide Alikamatwa Jumanne July 26 2016 nyumbani kwake Kinshasa kwa
tuhuma za kumshambulia dancer wake wa kike wakati wakiwa uwanja wa ndege
wa kimataifa wa Jomo Kenyata Nairobi na baadaye ikawa imeripotiwa kuwa
amehukumiwa kwenda jela miezi 18 na adhabu hiyo kutajwa kuwa haitakuwa
na faini.
Taarifa
zilizoripotiwa ni kwamba Koffi Olomide kaachiwa huru baada ya kutumikia
kifungo cha siku mbili kati ya miezi 18 aliyohukumiwa awali.
BBC
imeripoti kuwa kuachiwa kwa koffi Olomide kumekuja baada ya Mahakama ya
Kinshasa kusema kuwa hawakuona sababu za kutosha za kuhukumiwa kwa
Koffi Olomide kutokana na tukio alilofanya JKIA.
Pamoja
na baadhi ya vyombo vya habari Afrika kuripoti kwamba Koffi alihukumiwa
kifungo cha miezi 18 jela , Promoter wake wa nchini Kenya Jules Nsana
amekanusha madai hayo na kusema kesi dhidi ya Koffi ilikuwa bado iko
kwenye uchunguzi na kwamba baada ya uchunguzi wamebaini hakuna ushahidi
wa kutosha wa kumtia hatiani Koffi Olomide.
Promoter Jules amesema Olomide alimpigia simu akamtaka aombe msamaha kwa wakenya wote kwa niaba yake
Post a Comment