BINGWA WA KUBIKIRI WASICHANA NCHINI MALAWI ABAINIKA ANA UKIMWI........RAIS AAMURU AKAMATWE HARAKA
Rais
wa Malawi, Peter Mutharika juzi alitoa amri ya kukamatwa kwa Eric Aniva
ambaye hivi karibuni alibainika kufanya kibarua cha kuwabikiri mabinti
wa chini ya umri wa miaka 13 zaidi ya 100.
Amri hiyo ya Rais imekuja baada ya kubainika kuwa mwanamume huyo maarufu kwa jina la ‘Fisi’ anaishi na Virusi vya Ukimwi (VVU).
Mutharika
alisema lazima mwanamume huyo akamatwe na hatua kali zichukuliwe dhidi
yake kwa kuwa, kwa makusudi alifanya vitendo viovu akijua anaishi na VVU
na lengo lake lilikuwa kuwaambukiza mabinti hao.
Aniva
aliingia matatani baada ya kukiri katika mahojiano akijinasibu kuwa
anaendesha maisha kwa kuwabikiri mabinti na kwamba hulipwa kuanzia dola
nne za Marekani mpaka saba ambayo ni wastani wa Sh10,000 kwa kila mtu.
Mwanamume
huyo alisema wazazi wa mabinti huwa wanampa kibarua cha kuwavusha
kutoka utoto kuingia katika utu uzima na kwamba hatua hiyo ni sawa na
tambiko.
Post a Comment