EXCLUSIVE: SIMBA YAMRUDISHA LOGARUSIC JIJINI DAR ES SALAAM, APEWA KAZI YA KUIPIMA UWEZO
Kocha Zdravko Logarusic anarejea jijini Dar es Salaam, safari hii akiwa amepewa kazi ya kukipima kikosi cha Simba.
Logarusic maarufu kama Loga, anakuja nchini ndani ya siku chache akiwa ameongozana na kikosi chake cha Inter Club cha Angola.
Kikosi
hicho kitapambana na Simba katika mechi ya Simba Day ambayo itapigwa
Agosti 8, siku ambayo Simba itauwa inatimiza miaka 80.
Tayari Logarusic alikuwa amesema angetamani kukutana na Simba na kuwaonyesha kazi yake ilivyo bora.
Sasa Simba inanolewa na Kocha Joseph Omog raia wa Cameroon na imejichimbia mjini Morogoro.
Chini
ya kocha huyo, Simba imecheza mechi moja ya kirafiki dhidi ya Polisi
Morogoro iliyo daraja la kwanza na kuivurumisha kwa mabao 6-0.
Post a Comment