NMB YATOA VIFAA VYA HOSPITALI NA MADAWATI - NANYUMBU


Meneja wa kitengo cha biashara za Serikali wa NMB Kanda ya Kusini ,Mr.Haji Msigwa akimkabidhivifaa vya Hospitali   Mkuu wa Wilaya ya Nanyumbu Mhe. Festo Kiswaga kwa ajili ya Hospitali ya Wilaya ya Nanyumbu

Meneja wa kitengo cha biashara za Serikali wa NMB Kanda ya Kusini, Mr. Haji Msigwa akimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Nanyumbu Mhe. Festo Kiswaga  sehemu ya madawati yaliyotolewa kwa ajili ya Shule ya Msingi Likokona .

Wanafunzi wa shule ya msingi Likokona walioshiriki hafla ya makabidhiano
Benki ya NMB kwa kuelewa uhitaji wa vifaa vya hospitali na madawati katika jamii

inayoizunguka, imetoa vifaa vya hospitali vyenye thamani ya shilingi milioni tano kwa

ajili ya Hospitali ya Wilaya ya Nanyumbu pamoja na madawati sabini yenye thamani ya

shilingi millioni tano kwa Shule ya Msingi Likokona iliyoko Wilayani Nanyumbu, Mkoani Mtwara.

Msaada huo uliopokelewa na Mkuu wa Wilaya ya Nanyumbu Mhe. Festo Kiswaga,   ni

mwendelezo wa sera ya NMB ya kuchangia huduma za jamii ili kukabiliana na

changamoto zinazokabili sekta ya elimu na Afya.

Akitoa shukrani kwa niaba ya wakazi wa Nanyumbu.Mhe Kiswaga alisema “Msaada huu

ambao tumeupokea leo kutoka NMB, utasaidia kupunguza uhaba mkubwa tuliokua nao

kwa kipindi kirefu. Vifaa tiba vimekua havitoshelezi katika hospitali yetu lakini pia

madawati nayo imekua ni kilio kikubwa katika shule za hapa Nanyumbu. Lakini leo NMB

wamekua sehemu ya maisha yetu na hivyo wameweza kujua hitaji letu na kutusaidia.

Naomba kutoa shukrani za pekee kwa uongozi mzima wa NMB.
 (credt michuzi blog)

No comments

Powered by Blogger.