YANGA YATOA DOZI PEMBA, AJIBU ACHEKA NA NYAVU

Timu ya Yanga imefanikiwa kuifunga Kombaini ya Chakechake bao 1-0 katika mchezo wa kirafiki uliopigwa kwenye Uwanja wa Gombani, Alhamisi hii.
Yanga ambayo ipo Pemba ilipoweka kambi ikijiandaa kwa msimu mpya wa 2017/18 pamoja na mchezo wao dhidi ya Simba, Jumatano ijayo ilionyesha uwezo mzuri katika mtanange huo.
Katika mchezo huo ambao licha ya Yanga kutumia vikosi viwili, iliibuka na ushindi huo mwembamba kwa bao lililofungwa na mshambuliaji wake mpya, Ibrahim Ajibu katika dakika ya 25.
Kikosi cha Yanga kilichoanza; Rostand Youthe, Hassan Kessy, Gadiel Michael, Kelvin Yondani, Abdallah Shaibu ‘Ninja’, Raphael Daud, Thaban Kamusoko, Said Makapu, Emmanuel Martin, Donald Ngoma na Ibrahim Ajibu.
Kikosi kilichocheza kipindi cha pili ni Ramadhan Kabwili, Juma Abdul, Haji Mwinyi, Nadir Haroub, Abdallah Shaibu ‘Ninja’, Maka Edward, Juma Mahadhi, Baruan Yahya, Yussuf Mhilu, Said Mussa na Amissi Tambwe. 

No comments

Powered by Blogger.