Wachezaji wa Yanga wakifanya mazoezi.
Kuelekea mchezo wao wa Agosti 23, mwaka huu, tambo za upinzani baina ya Simba na Yanga zimeendelea kuwa kubwa ambapo sasa timu hizo zote zipo visiwani Zanzibar.
Simba na Yanga zinatarajiwa kukutana katika mchezo huo wa kuukaribisha msimu wa 2017/18 ambao utapigwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Kumekuwa na presha kubwa kuelekea mchezo huo kwa kuwa pande zote zinaamini vikosi vyao vipo sawa, Yanga wapo Pemba wakati Simba wapo Unguja.
Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili, Hussein Nyika amesema kikosi chao kipo Pemba kwa ajili ya kuendeleza maandalizi ya msimu huo mpya, lakini kuhusu Simba wao hawawafikirii kabisa.
Kikosi cha timu ya Simba.
Upande wa Mratibu wa Simba, Abbas Suleiman amesema kikosi chao kimeshatua Unguja kwa ajili ya kujiandaa na msimu mpya na kuhusu Yanga, hilo ni suala la mwalimu anaweza kuzungumza zaidi lakini maandalizi yapo vizuri kwa upande wake.
Upande wa mashabiki wa timu hizo wamekuwa wakitishiana mitandaoni na kila upande ukiona wenyewe upo vizuri na unaweza kufanya vizuri katika mchezo huo ubaina ya timu zao.
Post a Comment