REAL MADRID YAIMENYA TENA BARCELONA NA KUTWAA KOMBE LA SUPER CUP
Timu ya Real Madrid imeifunga Barcelona 2-0 katika dimba la Bernabeu na kutwaa kombe la Hispania la Super Cup kwa ushindi wa jumla wa magoli 5-1.
Mabingwa hao wa Hispania na Ulaya waliutawala mchezo huo wakicheza bila ya nyota wao Cristiano Ronaldo anayetumikia adhabu ya kutokucheza michezo mitano.
Marco Asensio, aliyefunga katika ushindi wa magoli 3-1 katika mchezo wa kwanza, aliipatia Real Madrid goli la kwanza kwa shuti la umbali wa yadi 25.
Karim Benzema aliinasa krosi ya Marcelo na kumgeuza beki Samuel Umtiti na kuipatia Real Madrid goli la pili huku Barcelona wakishindwa kabisa kufurukuta.
Cristiano Ronaldo akiwa anashangilia ushindi huku akiwa ameshika kombe
Lionel Messi akiwa na baadhi ya wachezaji wenzake wa Barcelona wakiwa hoi wasijue la kufanya baada ya kipigo
Post a Comment