RASMI SIMBA YATANGAZA KUMSAJILI NIYONZIMA, ATACHEZA SIMBA DAY
Hatimaye Klabu ya Simba imetangaza rasmi kumsajili Haruna Niyonzima ambaye aliichezea Yanga kwa misimu sita mfululizo.
Hatua hiyo imetangazwa na Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara alipozungumza na waandishi wa habari leo Jumanne.
Akizungumza zaidi, Manara alisema: “Yes Haruna ni mchezaji wa Simba, atakuja Simba, ukiona Rwanda Air imetua hapa ikiwa na wachezaji wa Simba jua naye atakuwemo kwa kuwa timu yetu itapitia Rwanda, au anaweza kuja mapema kabla ya wenzake waliopo Sauzi kambini.
“Bado yupo Rwanda kwa ajili ya mambo yake binafsi, ameshamaliza mkataba huko aliko kuwa akicheza na sisit umeshamalizana naye, kila kitu safi, atakuja na hata katika Simba Day atakuwepo.”
Post a Comment