RAIS MAGUFULI AMCHIMBA MKWARA MBUNGE WA CUF

        Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amempiga biti Mbunge na viongozi wa upinzani mkoani Tanga kutojisifia kuwa wao wameleta mradi wa Bomba la Mafuta katika eneo la Chongoleani Tanga.

Rais Magufuli amesema kuwa asitokee mtu yoyote katika jimbo hilo na kusema kuwa mradi huo wa bomba la mafuta ameuleta kwani mradi huo umeletwa na serikali ya Magufuli chini ya Chama Cha Mapinduzi.

“Hili bomba la mafuta lingeweza kwenda kokote hapa Tanga, tungeweza kulipeleka hata katika majimbo mengine ambayo yapo chini ya CCM lakini tumelileta hapa Chongoleani, sijui hata chama gani kwa sababu serikali yangu haibagui chama inataka kuleta maendeleo ya wananchi, hivyo tumeleta hili bomba la mafuta hapa ili kuleta maendeleo kwa wananchi asitokee mtu yeyote akasema amelileta hili bomba, ashindwe na alegee, limeletwa na serikali ya Magufuli” alisema Rais Magufuli. 

Aidha Rais Magufuli na Rais wa Uganda Museveni leo tarehe 5 Agosti 2017 wameweka jiwe la msingi la ujenzi wa Bomba la Mafuta kutoka Hoima, Kaskazini mwa Uganda hadi Chongoleani Tanga.
Kata ya Chongoleani Tanga ipo katika Halmashauri ya Tanga Mjini, jimbo ambalo lipo chini ya Mbunge Mussa Mbaruk kwa tiketi ya Chama Cha Wananchi (CUF).

No comments

Powered by Blogger.