Polisi kufunga CCTV Camera Dar es Salaam

 Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro akizungumza na Balozi wa Korea Kusini Song, Geum Young wakati wa siku maalum ya kuadhimisha urafiki kati ya Tanzania na nchi ya Korea kusini ambapo Balozi huyo amekubali kusaidia kufunga kamera maalum za kufuatilia wahalifu-CCTV katika jiji la Dar es Salaam. (Picha na Jeshi la Polisi)
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Korea Kusini Song, Geum Young (wa tatu kutoka kushoto) pamoja na maofisa wengine wakati wa siku maalum ya kuadhimisha urafiki kati ya Tanzania na nchi ya Korea kusini ambapo Balozi huyo amekubali kusaidia kufunga kamera maalum za kufuatilia wahalifu-CCTV katika jiji la Dar es Salaam.

Jeshi la Polisi nchini kwakushirikiana na nchi ya Korea Kusini lipo katika mpango wa kufunga kamera za usalama (CCTV Camera) katika mitaa ya jiji la Dar es Salaam ili kupunguza vitendo vya uhalifu pamoja na kupunguza idadi ya Askari wanaofanya doria
Hayo yamesemwa jijini Dar es Salaam na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro wakati wa maadhimisho ya siku ya urafiki kati ya Tanzania na Korea kusini ambayo imefanyika kwa kuwakutanisha baadhi ya Askari Polisi waliowahi kupata mafunzo ya Upelelezi katika nchi hiyo.
Aidha IGP Sirro amesema Jeshi la Polisi litaendelea kutilia mkazo katika kuwapatia mafunzo wataalamu wake wanaoshughulika na uhalifu kwa njia ya mtandao ili kuendana na kasi ya wahalifu wa njia hiyo ambapo amewataka Wananchi kuendelea kutoa ushirikiano ili kuweza kuwabaini wahalifu wanaotumia mitandao kufanya uhalifu wao.
Kwa upande wake Balozi wa Korea Kusini nchini Tanzania Song Geum-Young amesema kufungwa kwa kamera hizo kutasaidia kwa kiasi kikubwa kukabiliana na uhalifu ambapo amesema nchini Korea Kusini Kamera zimesaidia sana kupambana na vitendo vya uhalifu.

Nchi ya Tanzania na Korea kusini zimekuwa na ushirikiano katika Nyanja mbalimbali ambapo kwa Uapnde wa Jeshi la Polisi kila mwaka Askari wawili wamekuwa wakienda kujifunza katika Jeshi la Polisi la Korea Kusini.

No comments

Powered by Blogger.